SERIKALI YA VISIWA VYA SHELISHELI KUANZISHA KOZI YA UZAMIAJI

29 Jun, 2022
SERIKALI YA VISIWA VYA SHELISHELI KUANZISHA KOZI YA UZAMIAJI

Serikali ya Visiwa vya Shelisheli imesema inatarajia kuanzisha kozi ya Uzamiaji nchini Tanzania kwa kushirikiana na Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) haraka iwezekanavyo

Hayo yamesemwa na Balozi wa Visiwa hivyo Mhe. Maryvonne Pool wakati wa mjadala wa pamoja kati ya wawakilishi kutoka Visiwa vya Shelisheli na watumishi wa Chuo cha bahari Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha DMI tarehe 27.06.2022

Mjadala huo umelenga kupata uzoefu kutoka kwa wawakilishi wa Visiwa vya Shelisheli kuhusiana na Uchumi wa Bluu hususan shughuli za bahari na uvuvi ambao Visiwa hivyo tayari wameshaanza kutekeleza agenda ya Uchumi wa Bluu katika Taifa lao.

Katika majadiliano hayo, Balozi wa Visiwa vya Shelisheli nchini Tanzania Mhe. amesema nchi yake itaanzisha kozi ya Uzamiaji nchini Tanzania kwa kushirikiana na Chuo cha bahari Dar es Salaam (DMI) ili kuongeza fursa katika tasnia ya bahari.

Balozi wa Visiwa vya Shelisheli (Kusoto) akiweka saini katika kitabu cha wageni

Mkuu wa Chuo cha bahari Dar es Salaam Dkt. Tumaini Gurumo (Kulia) akikaribisha ujumbe kutoka Visiwa vya Shelisheli

Balozi wa Visiwa vya Shelisheli akitambulisha timu ya wataalam aliyoambatana nayo

Mtaalamu wa Sheria, Ulinzi na Usalama baharini kutoka Visiwa vya Shelisheli, Bi Sheryl Vangadasamy akitoa mada wakati wa mjadala

Wakuu wa Idara na Vitengo (DMI) wakisikiliza kwa makini